Willy Paul alimpa Jalang’o 400k kwa kukubali kukutana naye ▷ Kenya News

Huenda wampenda ama wamchukia, mwimbaji wa nyimbo za injili, Willy Paul, lakini yuko miongoni mwa wanamziki wa Kenya waliobobea ambaye pia amefanikiwa kiasi cha haja katika nyanja ya mziki.

Licha ya kupakua miziki mipya kila kuchao, kualikwa katika hafla kubwa na matamasha, Pozee amejiundia jina na mara kwa mara hutia mifukoni vitita vikubwa vya pesa.

Habari Nyingine: Sura ya mtoto wa Alikiba ni kama ya baba yake, wanafanana mfano wa shilingi kwa ya pili

Habari Nyingine: Polisi wawakamata washukiwa 4 sugu ambao wamekuwa wakiwaibia wateja pesa katika ATM

Kufanikiwa kwake kifedha kilithibitishwa na mcheshi tajika Jalango, ambaye alimsifu kupitia ukurasa wake wa Instagram mnamo Alhamisi, Juni 20, asubuhi.

Kulingana na Jalango, mwimbaji huyo anayetesa kwa wimbo Hallelujah, alichochomoa kitita kikubwa cha pesa na kumpa kama asante kwa kukubali kukutana naye.

Jalango alidokeza kuwa walikuwa wameagana kukutana na nyota huyo lakini kwa sababu shughuli nyingi, mkutano huo ukaahirishwa, jambo ambalo halikumkera Pozee.

Kwani alisubiri hadi Jalas alopopata nafasi ya kujumuika naye amabapo alichomoa KSH 400k kwa kukubali kukutana naye.

“Niliingia Sankara kukutana na Pozee aliyekuwa amezingiriwa na walinda wake wa usalama, wavulana wachache na wasichana wanne warembo sana. Kisha nikamuliza Mwana Mkunaji nikusaidi vipi? Kabla hata sijatamka neno lingine alinisukumia KSh 400k pesa taslimu na kuniambia ni ya kukubali kukutana naye,” Jalas alikariri.

Ni baada ya kumpokeza hela hizo ndipo staa huyo akawasilisha pendekezo lake la kutaka awe msimamizi wake rasmi wa hafla zake za ndani na nje ya nchi kwa muda wa mwezi moja.

Huku Jalango akitaka kujua kama mwimbaji huyo angewezana na gharama yake, Willy Paul aliraraua kijikaratasi kwenye hundi yake na kumtaka aandike kiasi cha pesa alichopenda kupewa kwa kazi hiyo.

Habari Nyingine: Nyota wa zamani wa Chelsea Fernando Torres rasmi astaafu soka

“Willy Paul aliniambia anataka niwe msimamizi rasmi katika hafla zake. Kwa sasa ana hafla 29 zilizoratibiwa kote ulimwenguni kuhudhuria. Ameratibiwa kitumbuiza watu nchi Afrka Kusini, Nigeria, tamasha nne nchini Tanzania, saba Uganda ana zingine kadhaa humu nchini. Katika ratiba yake ya usafiri, huwahusisha mpiga picha wake, wanasakata densi 14, designa na msamizi wake rasmi. Nilikubali lakini nilitaka kujua tarehe za tamasha hizo. Alitka kujua gharama kisha nikmwambia bei yangu sio rahisi, kisha alikata kijikaratasi kwenye kijatabu chake cha hunda na kunitaka niandike bei yangu. Huyo kijana yuko sawa Pozee nakubali kazi yako,” mcheshi huyo aliandika.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko


Posted

in

by

Tags: