Racheal Shebesh asisimua mitandao kwa kukata mauno Murang’a ▷ Kenya News

Racheal Shebesh aliwafurahisha wengi baada ya kuonekana kwenye video akisakata densi huku wimbo wake Diamond wa Tetema ukichezwa

-Licha ya umri wake, mwanasiasa huyo alionekana kuwa machachari na kuonyesha umahiri katika kunengua mauno

Aliyekuwa Mwakilishi wa Wanawake kaunti ya Nairobi Rachael Shebesh amewaacha wengi wakiwa wameduwaa baada ya kuonyesha umahiri wake katika usakataji densi.

Shebesh alisakata densi kule Murang’a na kuwaacha wengi wakimezea mate ubingwa wake katika kujilegeza na kuzungusha kiuno.

Habari Nyingine: Mbunge wa Jubilee amsuta rais Uhuru Kenyatta kwa kuwaita viongozi wa Mlima Kenya majambazi

Wakazi wa kaunti ya Murang’a wakiwa wamejawa furaha, walimtizama Shebesh akizungusha umbo lake la kuvutia kwa mitindo ya kisasa.

Huku DJ akimcheza densi ya aina ya Shaku, mwanasiasa huyo alionyesha wazi kuwa yeye aliwahi kuhudhuria ‘dunda’ ambazo ni maarufu miongoni ma vijana wa kisasa.

Habari Nyingine: Wazazi wa mapacha waliotenganishwa baada ya kuzaliwa kuishtaki hospitali ya rufaa ya Kakamega

Lakini ni wimbo wake Diamond wa Tetema ambao wachezaji densi huzikwenda chini kwa chini na ambao pia ulimpa Shebesh sifa kochokocho.

Mashabiki waliokuwa kwenye hafla hiyo walipendezwa sana na jazba ya muziki na kuwasha moto hewani.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko Newspaper


Posted

in

by

Tags: