Mwigizaji wa Aunty Boss, Sandra Dacha almaarufu Silprosa asema hawezi mchumbia jamaa hana hela ▷ Kenya News

Mwigizaji na mcheshi Sandra Dacha anatambulika kwa kupenda maisha na vitu vyenye thamani katika kipindi cha Aunty Boss.

Mwigizaji huyo alizua minong’ono mitandaoni kufuatia matamshi yake ya kutatanisha hewani yaliyozua mjadala mkali.

Habari Nyingine:

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na TUKO.co.ke, mwigizajo huyo alifichua kwamba hana mpango wowote wa kuanza maisha na mwanamme ambaye hana pesa wala mwelekeo maishani.

Kipusa huyo alitangaza msimamo wake huo pasi na kujali kile kitakachosemwa na watu kumhusu.

Mwigizaji wa Aunty Boss, Sandra Dacha almaarufu Silprosa asema huwezi mchumbiakama huna hela

Mwigizaji wa Aunty Boss, Sandra Dacha almaarufu Silprosa asema huwezi mchumbiakama huna hela
Source: Original

Wengi wamejiuliza ni kwa nini Sandra aliwahukumu wanaume kwa kiasi hicho lakini kwake yeye hayupo tayari kuolewa.

Kulingana na mcheshi huyo, wakati wa watu kuzungumza ukweli umewadia kwani hamna yeyote hapendi pesa.

Mwigizaji wa Aunty Boss, Sandra Dacha almaarufu Silprosa asema huwezi mchumbiakama huna hela

Mwigizaji wa Aunty Boss, Sandra Dacha almaarufu Silprosa asema huwezi mchumbiakama huna hela
Source: Original

“Mwanamke anastahili kutunzwa. Huwezi ishi na mwanamme ambaye hana kazi. Tusijitie hamnazo,” alidokeza.

Mwigizaji huyo alifichua kwamba angependa kuolea na mwanamme ambaye ana uwezo wa kumtunza na anamsaidia kifedha.

Mwigizaji wa Aunty Boss, Sandra Dacha almaarufu Silprosa asema huwezi mchumbiakama huna hela

Mwigizaji wa Aunty Boss, Sandra Dacha almaarufu Silprosa asema huwezi mchumbiakama huna hela
Source: Original

“Nitahisi vizuri iwapo mme wangu atanisaidia kulipa kodi ya nyumba wakati mmoja au mwingine. Sisemi anapaswa kunilipia kila wakati lakini ni bora ajaribu,” alieleza.

Sandra aliongeza kwamba mwanamme anayemfaa ni yule ambaye anajiweza kifedha.

“Naweza mchumbia tu mwanamme ambaye ana hela na anajiamini katika uhusiano wa kimapenzi. Iwapo anataka nionekane vizuri na nipendeze ni sharti nitumie hela zangu,” alifichua.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Posted

in

by

Tags: