Mwanamuziki Nandy akana madai kuwa ni kipenzi cha Willy Paul ▷ Kenya News

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Nandy amekanusha madai kuwa yeye na mwanamuziki wa humu nchini Willy Paul wanachumbiana

Nandy alidai kuwa mpenzi wake hayupo mahali popote humu duniani na kwamba Willy Paul ni rafiki wa kimuziki tu.

Akimjibu mfuasi mmoja kwenye ukurasa wa Instagram aliyetaka kujua iwapo yeye na Willy Paul ni wachumba, Nandy alisema mpenzi wake Ruge Mutahaba aliaga dunia na bado hajampata yule atakayejaza pengo alowacha.

Habari Nyingine: Gavana Sonko amzawidi mlinzi wake wa zamani KSh 300k siku ya harusi yake

Habari Nyingine: Oscar Sudi ashangazwa na kicheko cha Uhuru katika ngome za ODM na kilio Jubilee

Madai haya yanajiri siku chache baada ya wanamuziki hawa kuonekana kwa pamoja katika tamasha za hivi majuzi, moja iliyoandaliwa jijini Nairobi na nyingine kule Sumbwawanga nchini Tanzania.

Awali, Willy kupitia jumbe kadhaa kwenye mtandao wa Instagram alikuwa ameashiria kuwa yeye na Nandy ni wachumba, madai ambayo hakuyaweka wazi.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke


Posted

in

by

Tags: