Mtangazaji Ben Kitili na mkewe wamkaribisha mwanao wa pili miezi michache baada ya kufunga ndoa ▷ Kenya News

Mtangazaji wa KTN Ben Kitili na mkewe Amina Mude wamemkaribisha mwanao wa pili miezi michahche baada ya kufunga ndoa.

Tayari wawili hao wana mtoto mwingine wa kike ambaye ni kifungua mimba wao.

Habari Nyingine: Mtindo mpya wa nywele za Otile Brown wawasha moto mtandaoni

Amina alipakia picha ya mwanao wa kiume katika ukurasa wake wa Instagram akifichua kwamba alizaliwa mnamo Juni, 17 2019.

Awali, mkewe Ben aliandaa tamasha la kukata na shoka la kusherehekea ujio wa mwanawe na kuwaalika familia na marafiki ambao walimtunuku zawadi si haba.

Kipusa huyo amekuwa akishambuliwa na watu mitandaoni kufuatia hatua yake ya kuolewa na mwanahabari huyo.

Baadhi yao walimkashifu na kusema kwamba kwa kuwa yeye ni wa dini ya kiislamu hakupaswa kuolewa na mume wa dini nyingine yoyote.

Habari Nyingine: Tanzania: Wema Sepetu atatupwa kororoni siku 7 kwa kukaidi mahakama

Licha ya hayo, mwanadada huyo aliyapuuza yote hayo na kuendelea na maisha yake bila wasiwasi.

TUKO.co.ke inawatakia kila la heri wachumba hao.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko


Posted

in

by

Tags: