Msichana wa miaka 5 akataa kuingia chumbani mwao baada ya likizo ya kukata na shoka Dubai ▷ Kenya News

-Msichana huyo alisherehekea miaka 5 tangu azaliwe nchini Dubai

-Hata hivyo, baada ya kurejea kwao nchini Nigeria alisusia kuingia katika nyumba yao

-Alisalia nje huku akilia kwa kuwa hapakuwa na umeme

Video inayomuonesha msichana aliyesusia kuingia nyumbani kwao baada ya likizo ya Dubai imesambaa kwa kasi mitandaoni.

Msichana huyo aliyetambulika kama Anjola alikuwa amesherehekea miaka 5 tangu azaliwe nchini Dubai na kutokana na hatua hiyo ni bayana kwamba likizo hiyo ilikuwa ni ya kukata na shoka.

Habari Nyingine: AFCON 2019: CAF yachagua wakongwe 7 wa soka barani Afrika kuwa mabalozi

Msichana wa miaka 5 akataa kuingia chumbani mwao baada ya kutoka likizo Dubai

Msichana wa miaka 5 akataa kuingia chumbani mwao baada ya kutoka likizo Dubai. Picha: @ceolumineeofficial / Instagram Source: Instagram
Source: Instagram

Kwenye video hiyo, msichana huyo ambaye alikuwa akilia alisikika akilalama kwamba nyumba yao haikuwa na nguvu za umeme.

Habari Nyingine: DCI yasema wakili wa Philomena Mwilu anatumia uongo kortini kujinasua mtegoni

Mamake aidha anasikika akimsihi aingie chumbani humo.

Takriban dakika 40 hivi, Anjola aliingia chumbani humo baada ya mamake kumuahidi kwamba atampeleka Dubai tena kwa likizo mwezi utakaofuata.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko


Posted

in

by

Tags: