Mamake Diamond Platinumz amtia moyo Wema Sepetu saa chache baada ya kutupwa jela ▷ Kenya News

Mamake Diamond Platinumz, Sandrah Kassim amemtumia Wema Sepetu ujumbe wa kumtakia kila la heri saa chache tu baada ya kutupwa jela

TUKO.co.ke inafahamu kuwa mahakama iliamuru staa huyo wa filamu nchini Tanzania azuiliwe kwa siku saba akisuburi maamuzi ya dhamana yake.

Habari Nyingine: Gavana Sonko amzawidi mlinzi wake wa zamani KSh 300k siku ya harusi yake

Habari Nyingine: Oscar Sudi ashangazwa na kicheko cha Uhuru katika ngome za ODM na kilio Jubilee

Wema aliingia matatani baada ya kutohudhuria kwa mara mbii vikao vya kesi inayomkabili ambapo alikashifiwa kwa kuenezea video za ngono kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram mwaka wa 2018.

Hakimu mkazi Maira Kasonde aliamurisha kuwa Wema azuiliwe gerezani hadi Juni 24, 2019 ambapo kesi yake itasikizwa tena.

Wafuasi wake mitandaoni wamekuwa wakimtumia jumbe za kumtakia kila la heri na miongoni mwao ni mamake Diamond ambaye alimhakikishia kuwa mambo yatanyooka na kuwa shwari.

Habari Nyingine: Magazeti ya Kenya Jumatano, Juni 19: Magavana huwalipa mapasta KSh 1.7 milioni kila mwaka kuwaombea – SRC

” Usiwe na shaka, jitie nguvu kwani kila kitu kitakuwa shwari,” Ujumbe wa Mamake Diamond kwa Sepetu akiwa jela.

Itakumbukwa kuwa Sepetu aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond kwa miaka kadhaa kabla ya kutofautiana vibaya.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Source: Tuko.co.ke


Posted

in

by

Tags: