Juan Mata kutia saini mkataba mpya wa miaka 3 Man united ▷ Kenya News

– Juan Mata anatazamiwa kutia saini mkataba wa miaka mitatu Manchester United

– Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 utakwisha mwezi huu

– Mata alijunga na United akitokea Chelsea miaka mitano iliyopita

Manchester United wanaripotiwa kuwa katika harakati za mwisho kumpa nyota wao Juan Mata kandarasi mpya kumwezesha kukaa Old Trafford hadi msimu wa kiangazi wa mwaka 2022.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, kutoka Uhispania, mkataba wake wa sasa na klabu hiyo unapaniwa kutamatika mwishoni mwa mwezi huu, tangu kujiunga na timu hiyo miaka mitano iliyopita akitokea Chelsea mwaka wa 2014.

Habarai Nyingine: Manchester United mbioni kupata huduma za Neymar

Juan Mata kutia saini mkataba mpya wa miaka 3 Man united

Juan Mata nyota wa Man United kusalia kikosini.Picha: UGC
Source: Getty Images

Habari Nyingine: PSG tayari kumtema nyota wao Neymar

Kwa mujibu wa SunSport, ikinukuu ripoti za Daily Mirror, kiungo huyo wa kati, alitarajiwa kurefusha mkataba wake kwa mwaka mmoja baada ya kufanya majadiliano ya muda mrefu.

Hata hivyo, kulingana na taarifa zilizochapishwa na gazeti hilo, staa huyo alitaka kuongezewa mshahara zaidi kwa ule anaopokea wa sasa pauni 140,000 kila wiki.

Kulingana na taarifa zinazotoka katika klabu hiyo ni kuwa, sehemu zote mbili zimeafikiana kuhusu kumsajili Mata kwa mkataba mpya wa misimu mitatu.

Meneja wa ManU, Ole Gunnar Solskjaer, anaonekana kutokuwa na uhusiano mzuri na mchezaji huyo hasa baada ya kutofautina mwaka jana alipojiunga na kikosi hicho.

Huku kiungo huyo akisalia ugani Old Trafford, kwa miaka mingine mitatu, kandarasi yake hiyo ya pili itatamatika akiwa ametimia umri wa miaka 34.

Katika msimu uliopita, klabu hiyo iliwatema nyota Antonio Valencia, Ander Herrera na wengine kwa sababu ya umri huku Ashley Young akishikilia nafasi yake japo ya kuwa umri mmoja na nahodha wa zamani.

Habari Nyingine: Nataka mshahara wa pauni 300,000 kila wiki ndiposa nisalie Man U – Marcus Rashford

Duru zilikuwa zikiarifi kuwa Solskjaer, alikuwa na nia ya kuwasajili vijana chipukizi msimu mpya lakini anasemekana kuwa imara na huduma za Mata.

Awali TUKO.co.ke iliripoti kuwa Juan Mata alikuwa akilengwa na mabingwa wa Uhispania Barcelona na huenda angekatwa mshahara kama angeondoka United na kujiunga na Barcelona.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko


Posted

in

by

Tags: