Mtangazaji maarufu wa runinga ya Citizen Jeff Koinange alimuacha mwenzake Victoria Rubadiri kinywa wazi baada ya kutamka neno linalohusishwa na ufuska wakiwa hewani
Wawili hao walikuwa wakizungumzia matokeo ya vinasaba ya mapacha wa Kakamega ambao waligundulika kutenganishwa baada ya kuzaliwa miaka 19 iliyopita.
Habari Nyingine: Wazazi wa mapacha waliotenganishwa baada ya kuzaliwa kuishtaki hospitali ya rufaa ya Kakamega
Rubadiri alikuwa ameelezea jinsi mama wa wasichana hao atakavyokuwa na furaha kuwalea watatu hao ila kwa mshangao, Koinange alilitamka neno lililomuacha Rubadiri akiwa ameduwaa.
Koinange aliingiza neno ‘threesome’ ambalo hutumika sana kwa swala la ufuska ambapo watu zaidi ya wawili hushiriki tendo la ndoa.
Ilikuwa ni mshtuko mkubwa kwa Rubadiri kumskia Koinange akilitamka neno hilo mbele ya kamera huku mamilioni ya watu wakiwatazama.
Habari Nyingine: Ruto atamshinda Raila endapo uchaguzi utafanywa hii leo
Watumiaji wa mitandao ya kijamii bila kusita waligundua kuwa Rubadiri alikuwa ameshangazwa na tamko hilo na kwa upesi wakaanza kueneza video hiyo.
Wengi walishikilia kuwa semi za Koinange zilikuwa kimaksudi na zilinuia kutoa maana ya tukio la kushiriki ngono.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.
Source: Tuko News