Harmonize akana madai kuwa alimtongoza mpenzi wa Ben Pol, Anerlisa Muigai ▷ Kenya News

Mwanamuziki nyota wa Tanzania Harmonize amekanusha vikali madai kuwa alimtongoza mrithi wa kampuni ya Keroche Anerlisa Muigai ambaye pia ni mpenzi wa mwanamuziki Ben Pol

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Ben Pol alikuwa amefichua kupitia mtandao wa Instagram kuwa Harmonize amekuwa akimtumia Anerlisa jumbe za mahaba akiwa na nia ya kutaka kumpokonya.

Habari Nyingine: Sheria inamuonea ‘boy child’, majaji watatu wasema

Habari Nyingine: Nataka mshahara wa pauni 300,000 kila wiki ndiposa nisalie Man U – Marcus Rashford

Akiwa kwenye mahojiano na Zamaradi Mketema, Ben Pol pia aliwataja wanamuziki kadhaa akiwemo Shettah na rapa Khaligraph Jones akidai wamekuwa wakimmezea mate mpenzi wake.

Kati ya wanamuziki aliowakashifu kwa kutaka kumpokonya kipenzi chake, hakuna aliyezungumzia madai hayo ila inaonekana Harmonize alikwazika sana na kuamua kuvunja kimya chake.

” Ben Pol ni kakangu na nampenda sana, mapenzi huwa hayaeleweki, huwa inafika wakati ambapo mmoja anataka kujionyesha kwamba anamezewa sana mate na watu huko nje, najua Anerlisa alimweleza ili amtikise kidogo,” Harmonize alisema.

Habari Nyingine: Mapacha waliotenganishwa baada ya kuzaliwa wamesema hawataishtaki hospitali ya Kakamega

Aidha, Harmonize alidai ingelikuwa vema kwa Ben Pol kukabiliana naye ana kwa ana kuliko kusambaza madai kama hayo mitandaoni.

” Kama mwanaume kamili, angenijia tu na anieleze tatizo lake badala ya kutangaza mitandaoni, hapo alijiharibia sana. Mimi nilimjua Anerlisa kabla yeye kumjua na kama ningetaka kumchumbia basi ningemtongoza zamani sana, kuna mambo mengi ambayo yanaweza yakavunja uhusiano wa kimapenzi iwapo naeza yafichua ila sitaka kufanya hivyo,” Harmonize aliongezea.

Tayari Ben Pol amemposa Anerlisa na ni harusi tu ambayo wafuasi wao wanasubiri kwa sasa.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Source: Tuko Newspaper


Posted

in

by

Tags: