Gavana Sonko amzawadi mlinzi wake wa zamani KSh 300k siku ya harusi yake ▷ Kenya News

Bila shaka gavana wa Nairobi Mike Sonko ni mmoja wa wanasiasa tajiri zaidi humu nchini

Sonko kwa mara nyingi huonyesha ukarimu wake peupe na huwa na moyo wa kuwasaidia wale wasiojiweza.

Gavana huyo anayejulikana na wengi kwa kuishi maisha ya kifahari, aliwasha mitandao ya kijamii Jumamosi Juni 15, baada ya kumzawadi aliyekuwa mlinzi wake KSh 300,000 pesa taslimu.

Habari Nyingine: Nataka mshahara wa pauni 300,000 kila wiki ndiposa nisalie Man U – Marcus Rashford

Jambo lililowafurahisha wengi ni kwamba alimpatia noti mpya pekee ambazo zimezindulia hivi majuzi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Sonko alisema alihakikisha ameenda kwenye benki kuu kubadilisha noti za zamani na kupatiwa noti mpya .

TUKO.co.ke inafahamu kuwa Sonko alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliokuwa wamealikwa kuhudhuria harusi ya mlinzi wake wa zamani.

Habari Nyingine: Mapacha waliotenganishwa baada ya kuzaliwa wamesema hawataishtaki hospitali ya Kakamega

” Watu wanasema nina pesa nyingi kwenye nyumba yangu na kwamba noti za zamani zafaa kuondolewa, kwa hivyo sijaleta zile noti za zamani ila nilienda kwenye benki kuu na nikapatiana zile noti za zamani na nikabadilishiwa na hizi mpya, sasa nataka kuwapa maharusi noti hizi mpya kama zawadi,” Sonko alisema.

Aidha, hii sio mara ya kwanza kwa gavana Sonko kupatiana kitita kikubwa cha pesa kwenye hafla tofauti.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Source: Tuko.co.ke


Posted

in

by

Tags: