Bloga Robert Alai kuzuiliwa kwa siku 14 zaidi ▷ Kenya News

Bloga maarufu Robert Alai atazuiliwa kwa siku 14 zaidi akisubiri maamuzi ya dhamana yake

Alai alikamatwa Jumanne Juni 18, na maafisa kutoka idara ya upelelezi, DCI kwa kosa la kuchapisha mitandaoni picha za maafisa wa polisi walioangamia kwenye shambulio la kigaidi mjini Wajir.

Habari Nyingine: Maeneo ya Kati, Bonde la Ufa na Magharibi hayaungi sana mkono salamu ya Uhuru na Raila – Ipsos

Bloga Robert Alai kuzuiliwa kwa siku 14 zaidi

Bloga Robert Alai alikatwa kwa kosa la kueneza mitandaoni picha za maafisa wa polisi walioangamia kwenye shambulio la kigaidi Wajir
Source: Facebook

Habari Nyingine: Manchester United mbioni kupata huduma za Neymar

Kabla ya kukamatwa kwake, Msemaji wa Polisi Charles Owino alikuwa amemuonya Alai kwa kuchapisha picha hizo ila alikaidi onyo hilo.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, maafisa 12 wa polisi walifariki dunia baada ya gari walimokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetegwa ardhini na kulipuka.

Aidha, wanamgambo wa kundi ya kigaidi la al- Shabaab walidai kuhusika katika shambulio hilo.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko


Posted

in

by

Tags: