Afisa wa magereza Patrick Safari akamatwa kwa madai ya kusambaza picha za shambulizi la Wajir ▷ Kenya News

-Afisa huyo Patrick Safari hutumia ukurasa wake wa Facebook mara kwa mara na ana wafuasi wengi mno mtandaoni

-Inakisiwa kamba afisa huyo alimtumia bloga Robert Alai picha za waliouawa ambaye alizichapisha mtandaoni

-Bloga huyo alikamatwa Jumanne, Juni 18 na kuzuiliwa katika makao makuu ya ATPU

-Wawili hao watashtakiwa kwa kusambaza taarifa kuhusu shambulizi la kigaidi

Maafisa wa polisi wanamzuilia afisa wa magereza kwa madai ya kusambaza picha za maafisa wa polisi waliouawa katika shambulizi la kigaidi la kaunti ya Wajir Jumamosi, Juni 15.

Afisa huyo Patrick Safari alikamatwa na maafisa wa kupambana na ugaidi (ATPU) jijini Nairobi Mnamo Jumanne, Juni 18 kwa madai ya kusambaza picha hizo ambazo baadaye zilichapishwa mtandaoni na bloga Robert Alai.

Habari Nyingine: Gavana Sonko amzawidi mlinzi wake wa zamani KSh 300k siku ya harusi yake

Afisa wa magereza Patrick Safari akamatwa kwa madai ya kusambaza picha za shambulizo la Mandera

Afisa wa magereza Patrick Safari ana wafuasi wengi katika ukurasa wake wa Facebook. Picha: Patrick Safari/Facebook. Source: Facebook
Source: Facebook

Mawasiliano ya simu yaliwaelekeza maafisa hao katika mtaa wa kasarani ambapo walimkamata mshukiwa.

Safari ana wafuasi wengi katika ukurasa wake wa Facebook ambao unaonesha kuwa yeye huutumia mara kwa mara.

Maafisa wa kupambana na ugaidi walimkamata Alai Jumanne, Juni 18, kwa madai ya kuchapisha taarifa na kupakia picha hizo mtandaoni ambapo alisafirishwa hadi katika makao makuu ya ATPU.

Habari Nyingine: Oscar Sudi ashangazwa na kicheko cha Uhuru katika ngome za ODM na kilio Jubilee

Aliandamana na maafisa hao hadi makaazi yake ili kutafuta ushahidi zaidi kuhusiana na swala hilo.

Bloga huyo atafunguliwa mashtaka na iwapo atapatikana na hatia atafungwa kwa kusambaza taarifa kuhusu ugaidi.

Jumatatu, Juni 17, msemaji wa polisi Charles Owino alionya dhidi ya watu kusambaza picha za shambulizi hilo mitandaoni kwani itakuwa kama njia ya kuunga mkono kundi haramu la Al-Shabaab.

Takriban maafisa 8 walifariki wakati wa shambulzi hilo.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko


Posted

in

by

Tags: